Huku sehemu chache za Saudi Arabia zikipata
theluji kwa nadra, fatwa iliyotolewa ya kupiga marufuku kutengeneza sanamu
ya mtu kwa theluji ‘snowmen’ uliotolewa na kiongozi wa Kiislamu umekuwa
ukisambaa kwa kasi.
Uamuzi huo uliotolewa na Sheikh Mohammed Saleh al-Munajjid ambaye ni
maarufu sana unaonekana ulitolewa muda mrefu tu.
Sheikh huyo ametangaza kuwa kutengeneza sanamu huyo ni sawa na kutengeneza taswira
ya binadamu, jambo ambalo linapigwa marufuku na dini ya Kiislamu.
Uamuzi wake huo umekosolewa na wengi kwenye mtandao wa kijami wa Twitter,
huku raia kadhaa wa Saudia wameweka picha si tu za ‘snowmen’ lakini pia ngamia
kwa kutumia theluji na ma biharusi kwa theluji.
Chanzo: Mtandao wa Sheikh
No comments:
Post a Comment