Sunday, 11 January 2015
52 WAFARIKI DUNIA KWA KUNYWA BIA YENYE SUMU
Bia ya kienyeji iliyo na sumu imeua watu 52 Msumbiji, mamlaka za afya katika nchi hiyo iliyo kusini mwa Afrika zimesema siku ya Jumapili.
Watu wengine 51 walilazwa katika hospitali za wilaya ya Chitima na Songo kwenye jimbo la Tete kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, na 146 wamefika hospitalini kuchunguzwa iwapo wameathirika na sumu hiyo, afisa wa afya wa wilaya Alex Albertini ameiambia Redio Mozambique.
Wale waliokunywa bia hiyo walikuwa wakihudhuria msiba eneo hilo siku ya Jumamosi, alisema Albertini.
Pombe,jina la bia ya kienyeji ya Msumbiji, hutengenezwa kwa mtama au unga wa ngano.
Mamlaka husika zinaamini kinywaji hicho kilipata sumu kwa kutiliwa nyongo ya mamba wakati wa msiba huo.
Damu na bia za kienyeji zimepelekwa mji mkuu Maputo kufanyiwa uchunguzi, alisema mkurugenzi wa afya wa jimbo Carle Mosse.
Hakuna hata mmoja wa waombolezaji waliokunywa bia hiyo asubuhi waliolalamika kuumwa, lakini wale waliokunywa mchana, waliumwa, mamlaka zilisema.
Wanaamini bia hiyo lazima ilitiwa sumu wakati waombolezaji walipokuwa makaburini kuzika.
Mwanamke aliyetengeneza bia hiyo ni miongoni mwa waliokufa.
Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo.
Mamlaka za afya zimeanza kuchangia kwa kupeleka vyakula na vifaa vengine kwa familia zilizoathirika.
Chanzo: AP
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment