Ni pale ambapo mwanamke anachukua ujauzito kwa nia ya kumkabidhi mtoto kwa mtu mwengine baada ya kujifungua. Kwa kifupi, anabeba ujauzito kwa ajili ya wazazi wasio na uwezo wa kuzaa – wanajulikana kama “wazazi waliokusudiwa”.
Kuna aina mbili za kuchukua mimba kwaajili ya familia nyingine. Kwa desturi, yai la mama anayebeba hiyo mimba ndilo hutumika, ambapo hubaki kuwa mama aliye na asidi nasaba zake, yaani DNA. Aina ya pili, ni pale ambapo yai linatolewa na mama ambaye anataka msaada wa mtoto au mtu aliyejitolea. Yai linarutubishwa kupitia mchakato ambao yai hurutubishwa na mbegu za kiume nje ya mwili wake yaani kwenye maabara, IVF.
Ni halali?
Ina tofauti kutoka nchi hadi nchi
Nchi kama Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi na Bulgaria wanakataza kabisa mfumo wa aina wowote wa kubeba mimba.
Biashara ya ubebaji mimba ni halali katika baadhi ya majimbo ya Marekani, na nchi kama India, Urusi na Ukraine.
Watu wanaotaka kuwa wazazi huenda wakaenda nje ikiwa nchi zao za asili haziruhusu mchakato huo wa ubebabji mimba kwa niaba, au kama hawakufanikiwa kupata mwanamke anayeweza kuchukua mimba kwa niaba.
Hata hivyo, hata Australia sheria hubadilika. Kwa mfano, baadhi ya majimbo nchini humo ni kosa la jinai kwenda nchi nyingine kumtafuta mama atayebeba mimba kwa niaba tena kibiashara, wakati wengine huruhusu.
Watu huenda wapi kupata wa kubeba mimba kwa niaba?
Wataalamu wanasema nchi ambazo ni maarufu wa kuwa na akina mama walio tayari kuchukua mimba kwa niaba ni Marekani, India, Thailand, Ukraine na Urusi.
Mexico, Nepal, Poland na Georgia pia ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kuwa na uwezekano wa akina mama wa kutoa huduma hizo.
Gharama zinatofautiana katika kila nchi, na pia iantegemea na idadi ya mzunguzko wa IVF unaohitajika, na iwapo bima ya afya inahitajika.
- US - $100,000 (£60,000)
- India - $47,350
- Thailand - $52,000
- Ukraine - $49,950
- Georgia - $49,950
- Mexico - $45,000
Hakuna sheria zilizokusudiwa na kutambuliwa kwa wanaobeba mimba kwa niaba, kwahiyo wazazi wengi na watoto hubaki wakihaha na wengine hubaki bila utaifa.
Huchukua miezi chungu nzima kumrejesha mtoto aliyetokana na mama aliyebeba mimba kwa niaba, nyumbani kwao kwa asili, kwani huwa hawatambuliki moja kwa moja kama wazazi wao halali.
"Huko Thailand, mama wanaobeba mimba kwa niaba, wanaonekana kuwa mama halali, kwahiyo iwapo wazazi watamwacha mtoto na mama, basi yeye kisheria ana haki,” anasema Bi Scott.
"Huko India, wazazi waliokusudiwa kukabidhiwa mtoto huonekana kuwa wazazi halali, ambapo kutokana na sheria ya Uingereza, mama aliyebeba mimba kwa niaba, anatambulika kama mama halali.
“Hii inamaanisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyebeba mimba kwa niaba nchini India, kutokana na wazazi wa Uingereza, amezaliwa bila utaifa, na lazima aombe uraia wa Uingereza.”
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment