Monday, 19 January 2015

'WATOTO' WARUSHIWA MABOMU YA MACHOZI KENYA



Pupils protesting at Lang'ata school

Polisi wa Kenya wamerusha mabomu ya machozi kwa wanafunzi katika shule moja kubwa mjini Nairobi waliokuwa wakiandamana kupinga kuuzwa uwanja wao wa kuchezea kwa mwekezaji.

Wanafunzi hao walirejea kwenye shule yao ya Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili za mgomo wa walimu na kukuta eneo hilo la kuchezea likiwa limewekwa vizuizi.

Shule hiyo ina takriban watoto 1,000 kati ya umri wa miaka mitatu na 14 na kuendeshwa na baraza la mji wa Nairobi.

Watoto chungu nzima waliumizwa katika sekeseke hilo na polisi waliokuwa wakitawanya maandamano hayo na hivyo kupelekwa hospitali.

Baadhi waliwakabili polisi hao wa kuzuia vurugu, wakiwapungia fimbo.

Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa alipopigwa na jiwe lililorushwa na mmoja wa waandamanaji.

No comments:

Post a Comment