Friday, 9 January 2015

KIONGOZI WA DINI ABU HAMZA AFUNGWA MAISHA



 A courtroom sketch shows Abu Hamza, 56, with his defence lawyer Sam Schmidt 9 January 2015

Kiongozi wa kiislamu mwenye msimamo mkali Abu Hamza al-Masri amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama mjini New York kwa kuunga mkono ugaidi.

Alitiwa hatiani mwezi Mei kwa makosa mengi, ikiwemo utekajinyara na jaribio la kuunda kambi ya mafunzo ya kigaidi Marekani.

Kesi yake ilihusisha mchakato mrefu wa kuhamishwa kutoka Uingereza.

Wakati wa kutolewa hukumu, mawakili walimwomba jaji azingatie kuwa amepoteza mikono yake na jicho lake.

Pia walisema mpango wa kumfunga  Abu Hamza katika gereza kubwa la huko Colorado utakiuka ahadi Marekani iliwapa majaji wa London kumhamisha mwaka 2012.

Waendesha mashtaka siku ya Ijumaa walisema serikali ya Marekani haikuwahi kuweka ahadi kama hiyo kwa Uingereza na kifungo cha maisha ndio njia pekee.

No comments:

Post a Comment