Friday, 9 January 2015
SHAHIDI WA ICC KENYA 'AHUSISHWA NA UFISADI'
Mtu mmoja aliyekutwa amekufa Kenya aliyehusishwa na kesi ya Naibu Rais William Ruto alikutwa katika majaribio ya kuwahonga mashahidi, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC ilisema.
Waendesha mashtaka walisema hawakupanga kumwita, Meshack Yebei, kama shahidi kwasababu hiyo.
Mwili wa Bw Yebei ulikutwa magharibi mwa Kenya mapema mwezi huu.
Wakili wake alisema angetakiwa kuwa shahidi wa Bw Ruto, anayekana mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Bw Ruto alishtakiwa kwa ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa serikali kushtakiwa na mahakama iliyopo The Hague tangu ianzishwe zaidi ya muongo mmoja uliopita.
ICC ilifuta mashtaka kama hayo dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita, akidai mashahidi wa upande wa mashtaka wamekuwa wakitishwa na kubadilisha ushahidi wao.
Bw Kenyatta alisema hakuwa na hatia na pia upande wa mashtaka hawakuwa na kesi dhidi yake.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment