Sunday, 4 January 2015

AINA NYINGI ZA SARATANI NI 'BAHATI MBAYA'


 Lung cancer cells

Aina nyingi za saratani zinaweza kusemwa kuwa ni bahati mbaya badala ya kutokana na hatari kama vile uvutaji sigara, utafiti umeonyesha.

Wataalamu Marekani walikuwa wakijaribu kueleza kwanini baadhi ya mkusanyiko wa seli mwilini zilikuwa rahisi kupata saratani kuliko nyingine.

Matokeo hayo, kwenye jarida la Sayansi, zimeonyesha theluthi mbili ya aina ya saratani zilizofanyiwa utafiti zilisababishwa kwa bahati mbaya tu na si mtindo wa maisha.

Hata hivyo, baadhi ya aina za saratani zinazojulikana sana na zinazoua zinatokana na mtindo wa maisha.

Kwahiyo, je ni muda wa kushusha pumzi, kunywa na kula chochote bila kuwa na wasiwasi?

Haitoshangaza likiwa jibu ni Hapana.

Utafiti unaonyesha theluthi mbili ya aina ya saratani ni kwa bahati mbaya.

Lakini theluthi inayobaki kwa kiasi kikubwa kinatokana na mitindo yetu ya maisha.

Kunywa pombe kupindukia, muda mwingi juani au unene sana zote zinaweza kusababisha saratani.

Ikumbukwe 20% ya sababu za kupata saratani duniani ni kwa uvutaji sigara.

Utafiti huu ni ukumbusho kuwa saratani aghlabu ni bahati mbaya na njia pekee kuikwepa ni kuitambua mapema

No comments:

Post a Comment