Wednesday 7 January 2015

JINO LA MTU KUKUTWA KWENYE CHIPSI McDONALD


McDonald's Japan has apologised to customers and vowed to ensure product safety afterobjects including a tooth and plastic were found in its food    

McDonald imeomba radhi baada ya jino la binadamu kukutwa kwenye chipsi za mteja mmoja nchini Japan mwaka jana.

Mteja mmoja alitoa malalamiko baada ya kugundua hilo Agosti mwaka jana.

McDonald imesema uchunguzi huru uligundua kuwa ni jino la binadamu.

Kampuni hiyo pia imekiri kuwepo na plastiki ndani ya malai ‘ice-cream’ na ngozi ya plastiki ya kutengeneza mikoba ilikutwa kwenye kuku.

Wakurugenzi wa McDonald walisema watalifanyia kazi suala hilo ili matukio kama hayo yasitokee tena.

McDonald  imekabiliwa  na matatizo mengi Japan katika siku za karibuni, ikiwemo upungufu wa chipsi ambapo iliwalazimu kuagiza kutoka Marekani.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano, wakurugenzi hao walisema uchunguzi ulionyesha jino hilo halikupikwa.

“Hatujafanikiwa kugundua jino hilo liliingia vipi kwenye chakula," alisema.
Mwanamke aliyekuta jino awali alidai mfanyakazi mmoja alimwambia jino hilo lilikaangwa.

Chanzo: dailymail.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment