Sunday 4 January 2015

INDIA KUCHUNGUZA UTUMIAJI WA CHOO




Serikali ya India imetangaza kuwepo na mpango wa kitaifa wa kuangalia iwapo watu wanatumia vyoo.

Ni sehemu ya mpango wa taifa kufanya nchi hiyo iwe safi, uliozinduliwa na waziri mkuu mpya, Narendra Modi, miezi mitatu iliyopita.   

Wakaguzi wa usafi watafanya uchunguzi nyumba hadi nyumba wa namna watu wanavyotumia vyoo, na wakihifadhi matokeo kwenye simu za mkononi na vifaa vengine vya kiteknolojia.

Taarifa ya serikali ilisema hatua hiyo inaadhimisha utafiti wa awali ambao ulisimamia ujenzi wa vyoo.

Serikali hiyo ilisema imejenga vyoo nusu milioni tangu mwezi Oktoba.

Hatahivyo, Umoja wa Mataifa unaamini takriban nusu ya watu nchini India hawako radhi kutumia vyoo vya ndani, matokeo yake ni kuibuka kwa maradhi tele yanayohusu uchafu na vifo vya mapema.

Chanzo: Reuters na AFP


No comments:

Post a Comment