Sunday, 4 January 2015
TUMIA DAMU YA WALIONUSURIKA - WHO
Damu ya wagonjwa waliopona kutokana na Ebola inatakiwa kutumika kutibu wengine, Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza.
Afrika magharibi inakabiliwa na mlipuko mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya Ebola na zaidi ya watu 2,000 wamefariki dunia.
Kundi la wataalamu duniani wamekuwa wakikutana kutathmini tiba za majaribio zitakazoweza kutibu Ebola.
WHO pia imetangaza kuwa chanjo za Ebola zinaweza kutumika ifikapo mwezi Novemba.
Dawa ya damu
Watu hutengeneza kinga kwenye damukatika jaribio la kupambana na maambukizi ya Ebola
Kinadharia, kinga hizi (antibodies) zinaweza kuhamishwa kutoka mtu aliyenusurika kwa mtu mgonjwa ili kuipa nguvu mfumo wao wa kinga.
Hatahivyo, takwimu za kutosha za ubora wa tiba hiyo hazipo.
Utafiti uliofanyika katika mlipuko wa mwaka 1995 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilionyesha watu saba kati ya nane walipona baada ya kupewa tiba ya aina hiyo.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni maamuzi muafaka kwa wakati huu ambapo tiba yakinifu haijapatikana, kwa kuwa jaribio hili lilishaleta manufaa, nadhani inatia matumaini, waendelee hadi hapo kinga na/ama dawa kamili itakapopatikana.
ReplyDelete