Kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe (katikati) anaendelea na matibabu hospitali |
Kiongozi wa upinzani Tanzania, Freeman Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana kwenye mji mkuu Dodoma.
Msemaji wa chama chake cha Chadema amethibitisha tukio hilo kwa Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Amesema kiongozi huyo wa chama alikuwa akirejea nyumbani kwake siku ya Jumatatu washambuliaji walipomvamia na kumjeruhi mguu.
Mnadhimu mkuu wa upinzani Ester Bulaya alisema kuna mipango inafanyika kumsafirisha Mbowe kwa njia ya anga na kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi kutokana na shambulio hilo.
Viongozi mbalimbali wamemtembelea kiongozi huyo hospitalini akiwemo Naibu Spika, Dr.Tulia Ackson na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai.
Kulingana na mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa, alikuwepo nyumbani kwa mwenyekiti huyo jana jioni pamoja na Godbless Lema, Joseph Mbilinyi na John Heche.
Chanzo: BBC na https://bit.ly/3cOuOx7