Tuesday, 31 March 2015
BUHARI 'ANAONEKANA' KUONGOZA UCHAGUZI NIGERIA
Matokeo ambayo bado hayajakamilika kutoka uchaguzi wa Nigeria unaashiria aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari amepata kura zaidi kuliko rais wa sasa aliye madarakani, Goodluck Jonathan.
Hata hivyo, majimbo yenye watu wengi zaidi kama vile Lagos na Rivers bado matokeo hayakutangazwa rasmi.
Huku nusu tu ya majimbo ya Nigeria yakiwa yametangazwa, chama cha Jenerali Buhari cha All Progressives Congress (APC) kiliripotiwa kuwa na kura zaidi kwa milioni mbili.
Matokeo zaidi yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumanne.
Tume ya uchaguzi ya Nigeria (Inec) ilisitisha kutangaza matokeo Jumatatu usiku, baada ya kutoa matokeo ya majimbo 18 na mji mkuu Abuja.
Chama cha Rais Jonathan cha People's Democratic Party (PDP) kilipata kura 6,488,210 na cha APC cha Jenerali Buhari kimepata kura 8,520,436.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment