Soko la Bauchi lilishambuliwa na kupata hasara kubwa Desemba 2014 |
Genge la watu limempiga mwanamke mmoja mpaka kumwuua mjini Bauchi kaskazini-mashariki mwa Nigeria wakiamini alikuwa akitaka kujitolea mhanga, polisi na walioshuhudia walisema.
Mwanamke huyo – ambaye ni kijana – alishambuliwa alipokataa kupekuliwa kwenye geti la kuingilia la soko hilo. Hakukutwa na mabomu yoyote.
Mfululizo wa mabomu ya kujitoa mhanga kaskazini mwa Nigeria yamekuwa yakilaumiwa kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Kundi hilo linataka kushinikiza sheria za Kiislamu katika nchi hiyo.
Walioshuhudia walisema genge hilo lilimvalisha tairi lililonyunyuziwa petroli kwenye kichwa cha mwanamke huyo na kuliwasha moto baada ya kumpiga.
Polisi walisema alikuwa tayari amekufa kabla hawakufika kwenye eneo la tukio kumwokoa na kusambaza genge hilo. Hakuna yeyote aliyekamatwa.
Hali halisi ya mauaji yake hayako wazi. Ripoti nyingine zinasema mwanamke huyo aliyeuawa alikuwa kafuatana na mwanamke mwengine lakini wengine wanasema alikuwa na mwanamme.
No comments:
Post a Comment