Friday, 6 March 2015

MABAKI YA THOMAS SANKARA KUFUKULIWA

Thomas Sankara in 1986

Serikali ya Burkina Faso imeamuru kufukuliwa kwa mabaki ya Thomas Sankara, aliyekuwa rais wa nchi hiyo aliyeuawa katika tukio la kupinduliwa mwaka 1987.

Hatua hiyo inamaanisha mabaki hayo yanaweza kutambuliwa rasmi – ombi lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu na wafuasi wa Sankara, waliotaka ushahidi kuwa mabaki hayo yalikuwa yake.

Bw Sankara – anayeonekana kama Che Guevara wa Afrika – alizikwa haraka katika mapinduzi yaliyoongozwa na mrithi wake, Blaise Compaore.

Bw Compaore aliachia urais baada ya maandamano makubwa kufanyika Oktoba mwaka jana, 2014.

Alipokuwa madarakani, mahakama ya Burkina Faso ilizuia ombi la familia ya Bw Sankara kutaka mabaki ya mwili wake kufukuliwa.

Bw Compaore amekuwa akikana kuhusika katika mauaji ya Sankara, akisisitiza “mambo yote yako wazi” na hana “la kuficha”.

Chanzo: BBC                         
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment