Wednesday, 11 March 2015

MAJERUHI WA BASI LILILOUA 42 WAZUNGUMZIA UKAIDI WA DEREVA

 
MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI:

Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule Dominick Mashauri na Omega Mwakasege.

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37.


Ajali hiyo iliyotokea baada ya basi la abiria la kampuni ya Majinja Express lililokua likitokea Iringa likielekea Dar es Salaam liligongana uso kwa uso na lori lililokua likitokea Dar es Salaam likielekea Iringa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya watu 41 walioaga dunia, wanaume ni 33, wanawake 5 na watoto watatu.

Taarifa zaidi kutoka kwa watu walio katika eneo hilo zinasema kuwa miili ya maiti 32 bado haijatambuliwa na ndugu ama jamaa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, ameelezea chanzo cha ajali hiyo akibaini kwamba dereva wa lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara suala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana na basi hilo la kampuni ya Majinja Express.

Moja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Jackson Manga alisema kama dereva wa basi hilo angezingatia ishara za taa kali alizokuwa akiwashiwa na dereva wa lori hilo kwa vyovyote vile ajali hiyo isingetokea. Manga alisema katika eneo hilo lenye mteremko wa wastani, lori lilikuwa likipandisha na basi lilikuwa likishuka.

Alisema ukaidi wa dereva wa basi ulisababisha dereva wa lori aingie katika shimo kubwa katika eneo hilo hali iliyosababisha ashindwe kulimudu gari hilo kabla ya kuvaana uso kwa uso na basi hilo.

“Baada ya kuvaana, kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika loli hilo liliruka juu na kwa kishindo kikubwa, kubamiza na kufunika basi,” alisema.

Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Kevin Humphrey ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi alisema; “tulisikia mshindo mkubwa baada ya basi letu kugongana na lori hilo na mshindo huo ulisababisha na kontena iliyotoka kwenye lori hilo na kupiga juu ya basi letu.”

Ajali za barabarani zimekithiri nchini Tanzania. Mwaka 2014 watu zaidi ya 200 walifariki kutokana na ajali za barabarani. Ajali nyingi husababishwa na dharau na mwendo wa kasi wa madereva.
 
Chanzo: wavuti.com

No comments:

Post a Comment