Mmoja wa wanasiasa
maarufu wa upinzani nchini Burundi, Hussein Radjabu ametoroka gerezani.
Ametoroka na wafungwa wengine watatu na polisi wanne
wenye silaha, akiwemo mkuu wa usalama wa gereza hilo.
Haileweki aliwezaje kutoroka.
Bw Radjabu amekuwa akitumikia kifungo cha miaka 13 kwa
kupanga njama ya kuipindua serikali.
Kabla ya kukamatwa mwaka 2007, Hussein Radjabu, alikuwa
mshirika wa karibu wa Rais Pierre Nkurunziza na Mwenyekiti wa Chama Tawala.
Haya yanatokea wakati kuna hali ya wasiwasi wa kisiasa
nchini Burundi kabla ya uchaguzi unaotarajia kufanyika baadae mwaka huu.
No comments:
Post a Comment