Monday 9 March 2015

MTOTO AFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA MWALIMU


 Generic image of Cairo

Mtoto wa kiume wa shule moja mjini Cairo amefariki dunia baada ya kupata kipigo kutoka kwa mwalimu wake, wizara ya elimu ya Misri imesema.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 alikufa siku ya Jumapili “ baada ya kupigwa na mwalimu siku moja kabla”, taarifa kutoka wizara ya elimu ilisema.

Ilisema “uchunguzi wa haraka” ulianzishwa kujua mazingira ya kifo cha mtoto huyo na mwalimu alisimamishwa kazi.

Ripoti zilizomtaja mtoto huyo kuwa ni Islam Sharif, zilisema alipigwa kwa kutofanya kazi zake za shule ‘homework’.

Alikuwa na majeraha ya kichwani na damu kuvia kwenye ubongo, mkuu wa idara ya uchunguzi Hisham Abdel Hamid aliliambia shirika la habari la AFP.

Mwalimu huyo alisema “hakuwa na nia ya kumwuua lakini kupiga ni sehemu ya kumtia mtoto adabu”, gazeti la taifa la Al-Ahram Al-Masa'I liliripoti.

Desemba mwaka jana, Baraza la Taifa la Misri kuhusu watoto na wazazi wa kike lilisema mashambulio dhidi ya watoto yalizidi kwa 55% baina ya Januari na Oktoba ukilinganisha na wastani wa idadi ya miaka mitatu iliyopita.

No comments:

Post a Comment