Mchakato wa kwanza kufanikiwa duniani wa kupandikiza uume ‘transplant’ umeripotiwa kufanyika Afrika
kusini.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye
hatotambulishwa hadharani, alipoteza uume wake wakati wa mchakato wa kutahiriwa
kufanyika vibaya.
Madaktari mjini Cape Town walisema upasuaji huo ulifanikiwa na mgonjwa alikuwa na furaha na afya njema.
Kundi hilo la madaktari lilisema kulikuwa na mjadala mzito wa kujadili iwapo upasuaji huo, ambao si suala la kuokoa maisha kama ilivyo kwa upasuaji wa kupandikiza moyo, ulifuata maadili ya tiba.
Kumewahi kuwa na jaribio kama hilo, moja ikiwa China. Inasadikiwa kuwa upasuaji ulifanikiwa, lakini baadae uume huo haukufanya kazi.
Kubadilishiwa uume
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18
tayari alikuwa na uzoefu wa mapenzi alipotahiriwa.
Mchakato huo ni
sehemu ya kukua kutoka utoto kuingia ujana katika baadhi ya sehemu za Afrika
kusini.
Sherehe za jando Afrika kusini |
Alibaki na
sentimeta moja tu ya uume wake halisi baada ya kutahiriwa.
Madaktari Afrika kusini walisema wana watu wengi wanaohitaji kupandikizwa uume duniani kote.
Wengi, japo wengine husema mamia, ya vijana wa kiume hufariki dunia kila mwaka wakati wa sherehe za kutahiriwa.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Duh....mambo ya kushangaza haya.
ReplyDelete