Bw Chabane inasemwa alikuwa mshirika wa karibu na Rais Zuma na hapo kwenye picha yupo nyuma yake mwaka 2012 |
Waziri wa Afrika kusini, Collins Chabane, na maafisa wawili wa usalama wamekufa kwenye ajali ya gari.
Gari yao iligongana na lori kaskazini – mashariki mwa mji wa Polokwane.
Bw Chabane, aliyekuwa na umri wa miaka 54, alikuwa waziri wa huduma za umma, mwanachama wa chama tawala cha ANC na mshirika wa karibu wa Rais Jacob Zuma.
Alikuwa ni msimamizi wa mipango ya mazishi ya Bw Nelson Mandela.
Bw Zuma alisema alishikwa na “mshtuko mkubwa na mwenye huzuni” kwa kifo hicho cha ghafla ambacho ni “pengo kubwa kwa serikali na nchi kwa ujumla”.
No comments:
Post a Comment