Sunday 29 March 2015

KINYESI KUPITA KIASI MLIMA EVEREST



 Mount Everest

Kinyeshi kupita kiasi na mikojo huachwa ikijazana na wapanda mlima kwenye mlima Everest.

Jambo hilo linasababisha uchafuzi wa mazingira na huenda ukaeneza maradhi, alisema mkuu wa jumuiya ya wapanda mlima wa Nepal.

Ang Tshering anataka serikali ya Nepal kuwaambia wageni wote kuhifadhi uchafu huo  inavyostahili.

Alisema kinyesi na mikojo imekuwa “ikijazana” kwa miaka kadhaa maeneo ya kambi nne zilizopo.

“Wapandaji milima huchimba shimo kwenye theluji kama vile choo na kuacha uchafu huo hapo.”

Zaidi ya wapanda mlima 700 na wanaowaongoza hukaa takriban miezi miwili mlimani humo kila msimu, ambapo huanza mwanzoni mwa mwezi Machi na kumalizika mwezi Mei.

Baadhi ya wapanda milima hubeba mifuko maalum ya kuhifadhi uchafu huo kwenye kambi za juu zaidi, alisema.

Kwenye kambi za chini kuna maturubali maalum ndio kama vyoo, ambapo ina njia maalum ya kupitisha uchafu huo.

Serikali ya Nepal bado inatafuta suluhu ya tatizo hilo.

Sheria mpya zinamaanisha kuwa kila mpanda mlima lazima arudi na kilo 8 za uchafu wanaporudi chini.

Hicho ni kiwango ambacho wataalamu wanaamini mpanda mlima hutoa akiwa safarini.

Watu hao pia hulipa dola 4000, ambazo hawarudishiwi  kama watashindwa kutimiza masharti hayo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment