Tuesday, 10 March 2015
ALIYEKUWA MKE WA RAIS LAURENT GBAGBO AFUNGWA
Aliyekuwa mke wa rais wa Ivory Coast, Simone Gbagbo, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kushiriki katika ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Gbagbo, mwenye umri wa miaka 65, alishtakiwa kwa kuingilia usalama wa taifa.
Mume wake, aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, anasubiri kesi yake ianze kusikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Zaidi ya watu 3,000 walifariki dunia katika ghasia hizo za baada ya uchaguzi wa rais kufuatia aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo kukataa kukubali kushindwa na Alassane Ouattara.
Yeye na mume wake walikamatwa mwaka 2011 baada ya majeshi kuvamia handaki ambapo wawili hao walikuwa wamepata hifadhi kwenye mji mkuu, Abidjan.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment