Sunday 22 March 2015

WADANGANYIFU 300 WA MITIHANI WAKAMATWA INDIA



Indians climb the wall of a building to help students appearing in an examination in Hajipur, in the eastern Indian state of Bihar
Picha hizi zimewatia aibu mamlaka husika nchini India

Takriban watu 300 wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini India, mamlaka zilisema, baada ya ripoti kuibuka kuwa kulifanyika udanganyifu katika mitihani ya shule.

Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao walipigwa picha wakipanda kuta za shule kuwapa majibu.

Wengi waliokamatwa walikuwa wazazi. Takriban wanafunzi 750 walifukuzwa.

Takriban wanafunzi milioni 1.4 wanafanya mitihani katika jimbo hilo la Bihar peke yake – mitihani inayoonekana muhimu kwa kuwapa nafasi ya kujiendeleza katika fani mbalimbali.

Mamlaka bila shaka wameadhirika sana na udanganyifu huo, mwandishi wa BBC alisema, huku tukio hilo likizusha kejeli kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wanafunzi walionekana wakinakili majibu kwenye vikaratasi vilivyopenyezwa, na polisi waliokuwa nje ya vituo vya mitihani walionekana wakipewa hongo wageuke wakijifanya hawaoni.

No comments:

Post a Comment