Thursday, 5 March 2015
WALIOKUWA WASHIRIKA WA BW MUGABE WAMSHITAKI
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameshtakiwa kwa kuwafurumusha kimakosa waliokuwa maafisa wawili waandamizi wa chama tawala.
Wawili hao walifukuzwa kwenye chama Desemba na Februari kwa madai ya kuunga mkono jaribio la kumpindua.
Ruagare Gumbo na Didymus Mutasa wamefungua kesi Mahakama Kuu ya Zimbabwe wakitaka amri itolewe ya wao kurejeshwa Zanu-PF.
Bw Gumbo aliiambia BBC kuwa Rais Mugabe ni “dikteta” na anatakiwa kuachia madaraka.
Wanataka pia mahakama ifute mabadiliko ambayo Rais Mugabe aliwasilisha kwenye mkutano wa chama Desemba iliyopita.
Wakifanikiwa, waliokuwa watu wake wa karibu sana rais huyo wataweza kuitisha mkutano wa kipekee wa chama ambapo kiongozi mpya anaweza kuchaguliwa kumrithi Bw Mugabe mwenye umri wa miaka 91.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment