Bi harusi mmoja nchini India alichomoka kwenye harusi
yake baada ya bwana harusi mtarajiwa kushindwa kutatua swali dogo la hisabati,
kulingana na polisi wa Uttar Pradesh.
Bi harusi mtarajiwa alimwambia bwana harusi mtarajiwa kujumlisha 15 na sita.
Alipojibu 17, akaamua kuifutilia mbali harusi hiyo.
Ripoti zinasema familia ya bwana harusi mtarajiwa ilijitahidi kumshawishi bi harusi arejee, lakini akakataa akisema bwana huyo ni mjinga.
Polisi wa eneo hilo walijaribu kupatanisha familia hizo, hatahivyo pande zote mbili zilirejesha zawadi zote zilizotolewa kabla ya harusi.
Ndoa nyingi India ni za kupangwa na familia, na ni jambo la kawaida kwa bwana na bibi harusi kuoana bila kujuana hapo awali.
Bw Mohar Singh alipanga harusi ya binti yake aitwaye Lovely na Bw Ram Baran.
"Lakini kabla ya sherehe za harusi Lovely akagundua kuwa Ram Baran hana elimu yoyote na hivyo akakataa kuolewa," alisema.
Mohar Singh aliliambia shirika la habari la AP kuwa "familia ya bwana harusi ilituficha kuhusu elimu yake duni".
"Hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kulijibu swali hilo aliloulizwa," alisema.
No comments:
Post a Comment