Kibao hicho kilipata zaidi ya $5m kwa ajili ya Pharrell Williams (kushoto) na Robin Thicke |
Baraza la wazee Marekani limetoa uamuzi kuwa walioandika wimbo wa Blurred Lines – miongoni mwa wimbo uliovuma na kuuzwa kwa wingi duniani – ulinakiliwa kutoka kibao cha Marvin Gaye.
Baraza hilo liliamua kibao hicho cha mwaka 2013 cha Pharrell Williams na Robin Thicke kilikiuka hatimiliki ya kibao cha Gaye cha mwaka 1977 kiitwacho Got To Give It Up.
Familia ya mwimbaji huyo wa miondoko ya Soul ambaye sasa ni marehemu imepewa dola milioni 7.3 za usumbufu.
Mmoja wa binti zake Marvin Gaye Nona |
Thicke na Williams walikana kunakili kibao hicho, na wakili wao alisema uamuzi huo unaonyesha “uamuzi mbaya sana”.
Wakati huohuo, wakili wa familia ya Gaye aliiambia Rolling Stone kuwa walitaka kuzuia uuzwaji wa wimbo huo wa Blurred Lines.
Gaye alifariki dunia Aprili 1984, akiwaachia watoto wake hakimiliki ya muziki wake.
Watoto wake - Nona, Frankie na Marvin Gaye III – walimshatki Thicke na Williams mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment