Thursday, 12 March 2015

ZAIDI YA 'WAGANGA 200' WAKAMATWA TANZANIA


Albino boys in Tanzania

Zaidi ya waganga wanaotumia ramli na waganga wa kienyeji 200 wamekamatwa Tanzania katika msako wa kuwapata wauaji wa albino.

Mauaji hayo hufanywa kwa imani za kishirikina unaoshinikizwa na baadhi ya waganga kwa madai kuwa viungo vya albino vinaweza kukuletea utajiri na bahati pia.

Rais Jakaya Kikwete ameelezea mauaji hayo ya albino kama “ushetani” ulioutia aibu Tanzania.

Takriban albino 80 wa Tanzania wameuawa tangu mwaka 2000, Umoja wa Mataifa ulisema.

Serikali ilipiga marufuku waganga wote wanaopiga ramli mwezi Januari katika jitihada za kuzuia mashambulio ya ziada na utekaji nyara wa albino.

No comments:

Post a Comment