Monday, 2 March 2015

RAIS WA NAMIBIA APATA TUZO YA $5M



Hifikepunye Pohamba
Hifikepunye Pohamba alikuwa muasisi wa vuguvugu la ukombozi, Swapo

Rais wa Namibia anayeondoka madarakani Hifikepunye Pohamba ameshinda tuzo yenye thamani kubwa duniani, tuzo ya Mo Ibrahim kwa uongozi wa Afrika.

Tuzo hiyo ya dola milioni 5 ($5m) hutolewa kila mwaka kwa kiongozi aliyechaguliwa na wananchi na akaongoza vyema, kuimarisha maisha ya watu na kisha kuachia madaraka.

Lakini tuzo hii ni ya nne katika kipindi cha miaka mitano kutopatikana mshindi.

Bw Pohamba, aliyekuwa muasi na aliyepigania uhuru wa nchi yake, amehudumu kwa mihula miwili kama rais wa Namibia.

Alichaguliwa mwanzo mwaka 2004, halafu tena mwaka 2009.

Anatarajiwa kurithiwa na rais aliyechaguliwa, Hage Geingob.

Dk Salim Ahmed Salim, mwenyekiti wa kamati ya waliotoa tuzo, alisema chini ya uongozi wa Bw Pohamba, Namibia iliimarisha hadhi yake kuwa “ yenye demokrasia imara, ya kipekee pamoja na uhuru wa vyombo vya habari na kuheshimu haki za binadamu”.

No comments:

Post a Comment