Thursday, 19 March 2015

RAIS WA TUNISIA AAHIDI KUPAMBANA NA UGAIDI



Police officers stand outside the parliament in Tunis, 18 March 2015
Majeshi ya usalama yalivamia makumbusho hayo kusaidia raia

 Rais wa Tunisia ameapa kupambana na ugaidi “bila huruma”, kufuatia shambulio la bunduki kwenye jumba la makumbusho la Bardo katika mji mkuu Tunis lililoua watu 19

Watalii 17 waliuawa katika shambulio hilo, wakiwemo kutoka Japan, Italia, Cololmbia, Australia, Ufaransa, Poland na Hispania, maafisa walisema.

Raia wawili wa Tunisia, mmoja akiwa polisi, nao pia waliuawa kwenye shambulio hilo la Jumatano.

Majeshi ya usalama yameua wapiganaji wawili lakini wanaendelea kuwasaka washirika wao.


Maafisa walisema zaidi ya watu 40, wakiwemo watalii na raia wa Tunisia, wamejeruhiwa.      


No comments:

Post a Comment