Monday, 10 November 2014

MWANAMKE ABURUZWA UTUPU KWA PUNDA, INDIA



The 45-year-old woman (left) with a police officer
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 anatuhumiwa kumwuua mtoto wa ndugu yake
Mwanamke mmoja kaskazini mwa India amevuliwa nguo na kuachwa utupu kisha kuburuzwa hadharani na punda kwa amri ya wazee wa kijiji baada ya kushutumiwa kumwuua mtoto wa ndugu yake.

Baraza la kijiji katika wilaya ya Rajsamand pia iliagiza uso wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 upakwe rangi nyeusi.

Familia ya ndugu zake inamshutumu mwanamke huyo kwa mauaji. Polisi wamewakamata watu 39.

Amri zinazotolewa na mabaraza ya vijiji- yaitwayo panchayats- hazina haki yoyote kisheria lakini yanaheshimiwa sana vijijini.

Afisa mwandamizi wa polisi Shweta Dhankhad aliiambia idhaa ya Hindi ya BBC kuwa tarehe 2 Novemba, mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 45, Vardi Singh, alijiua katika kijiji cha Thurawad.

Siku tatu baada ya maziko yake, mke wake na ndugu wengine walikwenda polisi wakidai Bw Singh aliuliwa na shangazi yake.

Siku ya Jumamosi usiku, familia hiyo ilikwenda kwa baraza la kijiji na kukubali mwanamke/shangazi huyo alikuwa na hatia ya mauaji.

Kwa amri ya baraza hilo, mwanamke huyo alikatwa kipara na uso wake kupakwa makaa, akavuliwa nguo zote na kuburuzwa kijijini hapo kwa punda.

Waandishi wanasema wanawake mara kwa mara huvuliwa nguo hadharani maeneo ya vijiji vya India kwa nia ya kuwaadhibu na kuwadhalilisha.

No comments:

Post a Comment