Monday, 24 November 2014

MTOTO AUAWA NA POLISI AKIWA NA BUNDUKI BANDIA



 Tamir Rice
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 amepigwa risasi na polisi wa mji wa Cleveland nchini Marekani na kufariki dunia, baada ya kubeba kwa kile kilichokuja kujulikana ni bunduki bandia.

Polisi wamesema afisa mmoja alimfyatulia risasi mara mbili mtoto huyo baada ya kushindwa kutii amri ya kunyanyua mikono.

Kuna mtu alimripoti mtoto huyo kwa polisi kuwa alikuwa akitisha watu na bunduki hiyo lakini hakujua kama ni ya kweli au la.

Afisa mmoja alikuwa ndio kwanza yuko kwenye mwaka wake wa kwanza katika kazi hiyo ya jeshi la polisi, mwengine tayari alikuwa na uzoefu wa miaka 10.

Daktari wa kaunti ya Cuyahoga aliyemfanyia uchunguzi amemtambua mtoto huyo kuwa  Tamir Rice.

Mtoto huyo alipigwa risasi siku ya Jumamosi mchana na kufariki dunia hospitalini asubuhi ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment