Monday 24 November 2014

KAMPUNI YA UBELGIJI YA GFI YASHUTUMIWA DRC

A demolished medical centre in Democratic Republic of Congo (2009)

Kampuni ya uchimbaji madini ya Ubelgiji imekuwa “ikidanganya mfululizo” kuhusu kutumia tingatinga kuvunja mamia ya nyumba huko Jamhuri ya Kidemkrosai ya Congo, shirika la kutetea hakia za binadamu la Amnesty.

Ushahidi mpya ulionyesha shirika la Groupe Forrest International (GFI) lilisambaza tingatinga kubomoa nyumba karibu na mgodi wa shaba na kobalti, ripoti hiyo ilisema.

GFI, iliyokataa kuhusika na kubomoa nyumba hizo kinyume na sheria mwaka 2009, lazima walipe fidia, shirika la Amnesty limesema.

DRC ina utajiri wa raslimali, lakini raia wao wengi wanaishi kwenye umaskini.  

Inakadiriwa kuwa ina 34% ya akiba ya madini ya kobalti na 10% ya akiba ya shaba.

Mwendesha mashtaka wa serikali alifanya uchunguzi wa ubomoaji huo na kujaribu kuwashtaki waliohusika, lakini kuzuiwa na maafisa wa serikali kufanya hivyo, kulingana na ripoti ya Amnesty.

Kampuni hiyo ya madini ilijitoa huko DRC mwaka 2012 na sasa mgodi huo unamilikiwa na serikali.

No comments:

Post a Comment