Thursday 27 November 2014

GHANA YAKUMBWA NA KASHFA YA 'DAWA ZA KULEVYA'


map





Upande wa upinzani nchini Ghana umetoa wito wa kuwepo  uchunguzi wa bunge katika madai kuwa muuzaji mmoja wa dawa za kulevya aina ya cocaine alikuwa na uwezo wa kuingia katika sehemu maalum ya mapumziko ya rais kwenye uwanja mkuu wa ndege nchini humo.

Anayedaiwa kuwa muuzaji alikamatwa nchini Uingereza, huku maafisa watatu wamefunguliwa mashtaka Ghana.

Tukio hilo limekuwa gumzo miongoni mwa raia wa Ghana, wakati upinzani na chama tawala wakishutumiana kuhusu biashara ya dawa za kulevya.

Afrika magharibi ni njia kuu ya mpito ya kupitisha dawa hizo kimagendo barani Ulaya.

Serikali imekana kuhusika kwa namna yoyote na tukio hilo kwa kile redio za nchi hiyo zilivyoiita “kashfa ya cocaine”.

Rais John Mahama pia amekana vikali taarifa kuwa Bi Nayele Ametefe aliyekamatwa uwanja wa ndege wa Heathrow Novemba 9, ana uhusiano na familia yake.




No comments:

Post a Comment