Monday 17 November 2014

MAANDAMANO KUPINGA KUVULIWA NGUO, KENYA


Protest in Nairobi, Kenya, over a woman being stripped for wearing a miniskirt (17 November 2014)
Takriban watu 200 wameandamana katika mji mkuu Nairobi, nchini Kenya, baada ya kundi la wanaume kurarua nguo za mwanamke mmoja kwa kuvaa sketi fupi.

Waandamanaji walipiga kelele wakisema “Ona aibu” na kuweka maua kwenye kituo cha basi ambapo shambulio hilo lilipofanyika, mwandishi wa BBC Anne Soy aliripoti.

Katika maandamano mengine ya upinzani, takriban wanaume 20 nao walipiga kelele wakisema “Vaa nguo, hatutaki haya”.

Kenya ni nchi ambayo wanaharakati hulalamika kuwa haki za wanawake aghlabu hukiukwa.
Kundi la akina mama, Kilimani Mums, liliandaa maandamano hayo baada ya video kusambazwa ikionyesha shambulio hilo katika mitandao ya jamii.

Ilizua hasira miongoni mwa Wakenya na kupitia mitandao ya kijamii #MydressMychoice na  #strippingshame kwenye twitter siku ya Jumamosi na Jumapili.

Naibu rais wa Kenya William Ruto naye aliingia kwenye mjadala, akisema Kenya si jamii ya “kishamba”  na wanaume waliomvua nguo mwanamke huyo lazima wakamatwe.

Wote, wanaume na wanawake, baadhi wakiwa wamevaa sketi fupi, waliandamana kwenye kituo cha basi na ofisi za mkuu wa polisi David Kimaiyo, wakitaka kusimamisha ukatili dhidi ya wanawake.

Bw Kimaiyo ametaka mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kuwasilisha malalamiko rasmi kwa polisi ili tukio hilo lifanyiwe uchunguzi.

No comments:

Post a Comment