Monday 17 November 2014

BURKINA FASO YAMTAJA RAIS WA MPITO



Michel Kafando seen in 2008
Michel Kafando, hapa mwaka 2008 aliwahi kuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Burkina Faso

Viongozi wa kisiasa na wa kijeshi Burkina Faso wamemchagua aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Michel Kafando, kuwa rais wa serikali ya mpito.

Hatua hiyo imefuatiwa na kutiwa saini kwa azimio siku ya Jumapili wa mwaka mmoja wa mpito kuelekea kwenye uchaguzi.

Bw Kafando alikuwa mmoja wa wagombea wanne kwa nafasi hiyo, wakiwemo waandishi wa habari wawili na msomi mmoja.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Rais Blaise Compaore alipolazimishwa kujiuzulu tarehe 31 Oktoba wakati wa maandamano ya watu wengi.

Lt Kanali Isaac Zida, ambaye alijitangaza kiongozi wa taifa hilo la Afrika magharibi, aliahidi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.

Makubaliano                                     

Azimio hilo la mpito litashuhudia bunge la mpito na kiongozi wa mpito mpaka uchaguzi uanadaliwe mwakani.

Bw Kafando, mwenye umri wa miaka 72, alichaguliwa na jopo maalum lililotokana na viongozi wa dini, wa kijeshi, kisiasa, kiraia na wa kimila.

Makubaliano katika mji mkuu Ouagadougou yaliendelea mpaka alfajir ya Jumatatu.

Kazi ya kwanza ya Bw Kafando itakuwa kumtaja waziri mkuu ambaye atateua wanachama 25 wa serikali.

Bw Kafando, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na aliwahi kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa aliyeiwakilisha wa Burkina Faso, atazuiwa kugombea katika uchaguzi ujao.

No comments:

Post a Comment