Tuesday, 4 November 2014

KASHFA YA FEDHA MALAWI, SITHOLE AFUNGWA



US dollars (file photo)

Mahakama ya Malawi imemhukumu aliyekuwa mfanyakazi wa serikali, miaka tisa gerezani na kazi ngumu kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya rushwa maarufu kama “cashgate” nchini humo.

Mhasibu msaidizi Victor Sithole ni afisa wa pili kukutwa na hatia kutokana na suala hilo.

Alikutwa na hatia kwa wizi wa zaidi ya $66,000 (£41,000).

Takriban watu 70 wamekamatwa baada ya uchunguzi wa fedha uliofanyika mwaka jana kudhihirisha kuwa takriban dola milioni 60 zilichomolewa kwenye mfuko wa serikali.

Wafanyabiashara na wanasiasa wanadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wa serikali kulipia bidhaa na huduma ambazo hazijawahi kuonekana.

Mwandishi wa BBC alisema kukamatwa kwa Sithole Agosti mwaka jana kulianzisha kwa kile kilichokuja kuitwa “cashgate” – kashfa ya fedha mbaya kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Ilikuja kudhihirika mwezi mmoja baada ya mkurugenzi wa bajeti wa wizara ya fedha kwa wakati huo Paul Mphwiyo kupigwa risasi.

No comments:

Post a Comment