Sunday, 23 November 2014

'BOKO HARAM' WAUA WAUZA SAMAKI 48



 Aftermath of a Boko Haram attack in Kano state, 15 November 2014

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram imeripotiwa kuwa wameua watu 48 katika shambulio dhidi ya wauzaji samaki karibu na mpaka wa Chad.

Kundi la wauzaji hao walisema baadhi walikatwa shingo wakati wengine walifungwa kwa kamba na kuzamishwa katika ziwa Chad.

Shambulio hilo lilifanyika siku ya Alhamis, lakini taarifa hizo zimechelewa kujulikana kwasababu Boko Haram wameharibu mitambo ya simu za mkononi eneo hilo.

Ni shambulio la pili kubwa kufanywa na Boko Haram katika siku mbili.

Katika shambulio la Alhamis, wafanyabiashara hao walikuwa wakielekea Chad kununua samaki ndipo wanamgambo hao waliweka kizuizi karibu na kijiji cha Doron Baga, takriban kilomita 180 kaskazini mwa Maiduguri katika jimbo la Borno.

Abubakar Gamandi, mkuu wa umoja wa wauza samaki, alisema wanamgambo hao hawakutumia bunduki zozote.

“Washambuliaji hao waliwaua wauzaji hao kimya kimya bila kutumia bunduki kuzuia kuonekana na majeshi,” aliliambia shirika la habari la AFP.

No comments:

Post a Comment