Tuesday 25 November 2014

WAKENYA WAKIMBIA BAADA YA SHAMBULIO


Protesters in Nairobi (25 November 2014)

Mamia ya watu wamekimbilia uwanja mdogo wa jeshi katika mji wa Mandera nchini Kenya kukiwa na hofu ya wapiganaji kuanzisha mashambulio upya.

Wengi waliokimbia nia wafanyakazi wa serikali wasio Waislamu wanaotaka serikali iwaondoshe eneo hilo, mwandishi wa habari wa BBC alisema.

Kundi la al-Shabab linalohusishwa na Al-Qaeda liliua watu 28 kwenye shambulio la basi siku ya Jumamosi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anapata shinikizo kubwa kusimamisha mashambulio hayo.

Makao makuu ya Al-Shabab yako nchi jirani ya Somalia, lakini limeanzisha mashambulio Kenya tangu mwaka 2011, baada ya Kenya kupeleka majeshi mpakani kusaidia kupambana na wapiganaji.

Mwandishi wa BBC aliyopo kwenye mji mkuu, Nairobi, alisema upinzani na baadhi ya wabunge wa chama tawala wametoa wito wa idara ya usalama kubadilishwa kabisa, ikiwemo kufukuzwa kwa waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku na mkuu wa polisi David Kimaiyo.
 

No comments:

Post a Comment