Sunday, 23 November 2014

GORDON BROWN 'KUACHIA NGAZI KAMA MBUNGE'



 Former Prime Minister Gordon Brown speaks at a campaign event in favour of the union in Clydebank, Scotland, September 16
Aliyekuwa waziri mkuu Gordon Brown anatarajiwa kuachia ngazi kama mbunge katika uchaguzi mkuu ujao, ripoti zinasema.

Mbunge huyo wa Kirkcaldy na Cowdenbeath atatangaza uamuzi wake huo “katika siku chache zijazo”, mshirika mmoja aliliambia gazeti la Sunday Mirror la Uingereza.

Hakuna uthibitisho wowote rasmi lakini viongozi waandamizi wa chama cha Labour wameiambia BBC wanatarajia ang’atuke.

Bw Brown mwenye umri wa miaka 63, ambaye alikuwa mstari wa mbele hivi karibuni katika kampeni dhidi ya uhuru wa Uskochi, amekitumikia chama hicho takriban miaka 32.

Alikuwa waziri mkuu tangu mwaka 2007 hadi 2010, chama cha Labour kiliposhindwa, tena katika matokeo mabaya kuwahi kutokea tangu mwaka 1983.

Kufuatia kushindwa huko, amekuwa haonekani sana bungeni tangu wakati huo.

No comments:

Post a Comment