Tuesday 11 November 2014

MAZISHI YA KITAIFA KWA RAIS WA ZAMBIA


 The coffin of Michael Sata being brought into the National Heroes Stadium in Lusaka, Zambia
Zambia imefanya mazishi ya kitaifa kwa ajili ya Rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwezi uliopita kwenye hospitali moja nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 77.

Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi hayo katika uwanja wa taifa wa Mashujaa kwenye mji mkuu, Lusaka.

Akijulikana kama “King Cobra” kwa ulimi wake mkali, Bw Sata alichaguliwa kuwa Rais wa Zambia mwaka 2011.

Nchi hiyo kwa sasa inaendeshwa na rais anaye kaimu, na uchaguzi upya unatarajiwa kufanyika mwezi Januari.

Mwandishi wa BBC aliyopo Lusaka Dennis Okari amesema ni shughuli yenye hisia kali.
Katika wiki iliyopita, raia wa nchi hiyo wametoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kiongozi wao – wakipita pembeni ya mwili wake uliokuwa umelazwa kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano Mulungushi.

Alifariki dunia siku chache baada ya Zambia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka Uingereza.

Alikuwa rais wa pili wa Zambia kufa akiwa madarakani

No comments:

Post a Comment