Tuesday, 18 November 2014
MUUAJI WA MAREKANI ARUHUSIWA 'KUOA'
Muuaji kutoka Marekani Charles Manson, mwenye umri wa miaka 80, imeripotiwa kuwa atapewa leseni ya kumwoa mwanamke wa miaka 26 aliyekuwa akimtembelea gerezani.
Leseni ya ndoa hiyo ilitolewa siku 10 zilizopita kwa Manson na Afton Elaine Burton, shirika la habari la AP limeripoti.
Bi Burton alihamia Corcoran, California, miaka tisa iliyopita ili awe karibu na gereza la Manson.
Manson anatumikia kifungo cha maisha kwa mauaji ya watu saba na mtoto mmoja ambaye alikuwa bado kuzaliwa mjini Los Angeles mwaka 1969.
Kati ya aliyowaua ni muigizaji aliyekuwa mjamzito Sharon Tate, mke wa mtayarishaji filamu Roman Polanski.
Bi Burton, anayejiita Star, aliiambia AP kuwa yeye na Mason wataoana mwezi ujao. Leseni hiyo ina uhalali wa siku 90.
"Nampenda," aliongeza.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment