Sunday, 2 November 2014

RISASI ZARINDIMA BURKINA FASO



People gather at the podium of the state TV headquarters in Ouagadougou, Burkina Faso, 2 November 2014
Waandamanaji wakiwa kituo cha televisheni cha taifa wakitarajia upinzani kutangaza lolote

Televisheni ya taifa ya Burkina Faso imetolewa hewani, muda mchache baada ya askari kufyatua risasi kwenye makao yake makuu, na kuwalazimisha waandamanaji na waandishi wa habari kutawanyika.

Wakati huo huo kwenye mji mkuu, Ouagadougou askari waliwatawanya maelfu ya waandamanaji na kuweka vizuizi eneo hilo.

Askari walishika madaraka siku ya Ijumaa baada ya kiongozi wa muda mrefu Blaise Compaore kuachia ngazi kufuatia maandamano ya siku kadhaa.

Umoja wa Mataifa umelaani jeshi kuchukua hatamu na kutishia kuweka vikwazo.

Mjumbe wa Afrika magharibi Mohamed Ibn Chambas alisema jeshi lazima liruhusu uongozi wa kiraia.

Jeshi lilimtangaza Lt Kanali Isaac Zida kuwa kiongozi wa serikali ya mpito siku ya Jumamosi.

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika maeneo mbalimbali mjini Ouagadougou siku ya Jumapili kulipinga jeshi.

Opposition leader Saran Sereme adjusts her headscarf as she visits the national television headquarters in Ouagadougou on November 2
Kiongozi wa upinzani Saran Sereme alipofika kituo cha televisheni cha taifa kabla tu risasi kufyatuliwa

Kulikuwa na tafrani wakati kiongozi wa upinzani Saran Sereme na aliyekuwa waziri wa ulinzi Kwame Lougue walipowasili kwenye makao makuu ya televisheni hiyo ya taifa.

Watu hao waliokusanyika waliamini Be Sereme alikuwa anatarajia kutangaza kuongoza serikali hiyo ya mpito, mwandishi wa BBC aliyopo Ouagadougou Laeila Adjovi aliripoti.

Taarifa zinasema Jenerali mstaafu Lougue naye alikusudia kutangaza kutaka kuongoza nchi hiyo wakati huo pia.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuwasili, risasi zikaanza kurushwa hivyo wafanyakazi na waandamanaji wakaanza kukimbia.


No comments:

Post a Comment