Monday, 10 November 2014

WABIDUN WA KUWAIT 'KUPEWA URAIA' WA COMOROS



Stateless Arabs, known as Bidun, demand Kuwaiti citizenship and basic rights, in Jahra. 2 October 2013
WaBidun wamekuwa wakiomba uraia wa Kuwait kwa muda mrefu, jambo linalopingwa na serikali
Maelfu ya watu wasiokuwa na uraia/utaifa nchini Kuwait – wajulikanao kama Bidun- huenda wakapewa uraia wa visiwa vya Comoro vilivyopo barani Afrika, afisa mmoja alisema.

Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya ndani aliliambia gazeti moja nchini humo kuwa watu hao wa Bidun watapewa uraia maalum wa kiuchumi kwenye visiwa hivyo.

Alisema wale watakaokubali watapewa vibali vya ukaazi nchini Kuwait.

Zaidi ya Wabidun 100,000 wanadai uraia wa Kuwait lakini huchukuliwa kama wakazi wanaokaa kinyume cha sheria na serikali hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, wamekuwa wakiandamana wakitaka uraia wa Kuwait na polisi wamekuwa wakiwatawanya kwa nguvu. Mamia wamekamatwa.

Serikali ya Kuwait imesema ni WaBidun 34,000 wenye sifa za kufikiriwa iwapo wapate uraia wa Kuwait au la.

Wengine huchukuliwa kama raia wa nchi nyingine ambao huenda walihamia Kuwait baada ya kugunduliwa kwa mafuta miongo mitano iliyopita au vizazi vya wahamiaji hao.

Serikali ya visiwa vya Comoro hadi sasa hawajasema lolote kuhusiana na ripoti hiyo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment