Thursday, 27 November 2014

MABINTI WAWILI WA INDIA 'WALIJINYONGA'



Villagers collect near tree where the girls were found in Badaun
Wanavijiji wenye hasira waliandamana kwenye mti ambapo mabinti hao walikutwa wamenyongwa wilaya ya Badaun
Mabinti wawili wa India waliokutwa wakining’inia kwenye mti mwezi Mei inasemwa kuwa walijiua na hawakubakwa na watu wengi kisha kuuliwa, wachunguzi wa serikali walisema.

Uamuzi huo umetolewa baada ya uchunguzi wa miezi kadhaa uliofanywa kufuatia shinikizo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Wanaume watatu waliokamatwa kuhusishwa na tukio hilo katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa nchi hiyo waliachiwa kwa dhamana mwezi Septemba.

Haiko wazi kwanini mabinti hao walijiua. Waandishi wanasema kuna maswali mengi yasiyo na majibu.

Wanaharakati wa masuala ya wanawake wanasema hawajaridhika na matokeo hayo na kutaka chombo hicho cha CBI kiendelee na uchunguzi.

Ndugu hao wawili, wanaodhaniwa kuwa na umri wa miaka 14 na 15, walikutwa wamejinyonga kwenye mwembe Mei 28.

Hali ya kuwepo maelezo machache ya sababu za mabinti hao kujiua kumesababisha wengi kuhoji matokeo hayo ya CBI.

No comments:

Post a Comment