Rais wa Indonesia amesababisha kitahanani kwa kupanda ndege daraja la ‘Economy’ kuelekea Singapore kuhudhuria mahafali ya kidato cha sita ya mtoto wake wa kiume.
Joko Widodo na mkewe walikataa kuchukua ndege ya Rais kwasababu ilikuwa safari ya binafsi.
Wawili hao walijilipia tiketi, japo serikali imelipia gharama za walinzi waliofuatana nao.
Baadhi ya wachunguzi wamemsifu Bw Widodo, wengine wanasema ni kutaka tu kupata umaarufu.
Rais wa Indonesia, Joko Widodo, akichukua selfie na wanafunzi katika shule ya mwanawe mjini Singapore |
Baba au rais?
Rais wa Indonesia na mkewe, Iriana, walienda kwenye mahafali ya mtoto wao wa mwisho, ambapo rais huyo alipiga picha za ‘selfie’ na wanafunzi wengine.
Walisafiri na ndege ya taifa, Garuda Indonesia, siku ya Ijumaa, na kupanga foleni kusubiri nyaraka zao zikaguliwe mjini Jakarta na abiria wengine, hivyo kusababisha abiria wengi kumshangaa.
"Rais anasafiri kama baba, si mkuu wa nchi, “ alisema afisa mmoja wa Indonesia, akielezea safari hiyo ya aina yake kwa mtu kama Rais.
Joko Widodo - anayejulikana kwa jina la Jokowi – alijijengea taswira ya mtu wa watu, kwanza kama meya wa mji wa Solo halafu kama gavana wa Jakarta.
No comments:
Post a Comment