Saturday, 15 November 2014
HAKUNA TENA EBOLA DRC
Mlipuko wa miezi mitatu wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeisha baada ya kusababisha vifo vya watu 49, waziri wa afya wa nchi hiyo alisema.
Felix Kabange alisema hakuna wagonjwa wapya waliosajiliwa tangu tarehe 4 Oktoba.
Mlipuko huo nchini humo hauhusiani kabisa na ule wa Afrika magharibi uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 5,000.
Ebola kwa mara ya kwanza uligunduliwa mwaka 1976 karibu na Ebola River ambapo sasa ndio Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Tangazo hilo la Jumamosi limetolewa baada ya mtu wa mwisho kupata ugonjwa huo nchini humo siku 42 zilizopita.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment