Saturday, 22 November 2014

SHAMBULIO LA BASI KENYA LAUA 28



Archive photo of al-Shabab fighters, 2011
Al-shabab limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya

Wanaoshukiwa kuwa wanachama kutoka kundi la Kisomali la al-Shabab wameua takriban watu 28 katika shambulio la basi kaskazini mwa Kenya, maafisa walisema.

Basi hilo lilikuwa linaelekea mji mkuu, Nairobi, liliposimamishwa kwenye kaunti ya Mandera, karibu na mpaka wa Somalia.

Watu hao wenye silaha waliwatenganisha wale waliodhani si Waislamu kabla ya kuwaua, kulingana na maafisa walioambiwa na walioshuhudia.

Al-Shabab, ambalo limekuwa likifanya mashambulio nchini Kenya tangu mwaka 2011, limekiri kufanya shambulio hilo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao unaohusishwa na kundi hilo limesema shambulio hilo limefanywa katika hali ya kulipiza kisasi kutokana na uvamizi wa polisi katika misikiti mjni  Mombasa mapema wiki hii.

No comments:

Post a Comment