Wednesday 19 November 2014

'BANGI' KUZINDULIWA NA FAMILIA YA BOB MARLEY




California Heritage Market in Los Angeles, California in this file photo taken July 11, 2014.
Familia ya marehemu wa aliyekuwa mwimbaji wa miondoko ya reggae, Bob Marley imezindua kwa kile walichoeleza toleo la kwanza duniani la bangi (Cannabis).

Itaitwa Marley Natural na itatumika kuuza mafuta ya kujipaka mwilini yaliyo na bangi na vipodozi vengine.

Bidhaa hiyo inatengenezwa na Privateer Holdings iliyopo katika jimbo la Washington, ikithamini maisha na urithi wa bidhaa muhimu ya Jamaica.

Inatarajiwa kuuzwa Marekani na ikiwezekana duniani kote kuanzia mwakani.

Binti yake Bob Marley, Cedella Marley, alisema baba yake angefurahi sana kwa hatua hiyo.

“Baba yangu angefurahi sana kuona watu wakielewa nguvu ya kuponya ya majani haya,” alisema.

Mkurugenzi mkuu wa Privateer Brendan Kennedy alisema Marley alikuwa mtu , ambaye kwa namna nyingi, alisaidia kuanzisha harakati za kuzuia kupigwa marufuku kwa bangi miaka 50 iliyopita.

Bob Marley alikufa kwa saratani Mei 1981. Alitumia bangi kama kiungo muhimu cha imani za Kirasta.

Utumiaji wa bangi (Cannabis) kwa ajili ya kujifurahisha ni halali Marekani katika jimbo la Colorado na Washington.

Majimbo mengine huenda yakafuata mkondo huo na mengine yanaruhusu uuzaji wa marijuana kwa ajili ya matibabu.




Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
        

No comments:

Post a Comment