Wahamiaji wasio na nyaraka halali wakisikiliza hotuba ya Rais Obama huko Philadelphia |
Mamilioni ya wahamiaji wanaoishi kinyume naa sheria Marekani wataruhusiwa kuomba kibali cha kufanya kazi katika mtikisiko mkubwa uliotangazwa na Rais Barack Obama.
Inahusisha wahamiaji walioishi Marekani kwa miaka mitano wenye watoto wanaoishi kihalali nchini humo.
Takriban watu milioni tano wanatarajiwa kufaidika kutokana na mabadiliko hayo aliyolazimisha kutumia madaraka yake, inayomruhusu Bw Obama kuliruka bunge la Congress.
Chama cha Republican kimemshutumu rais huyo kwa “madaraka ya kunyakua kwa nguvu isivyo halali”.
Inakadiriwa kuwepo wahamiaji haramu milioni 11 Marekani.
Katika mpango wa Bw Obama, wazazi ambao hawana nyaraka halali ambao watoto wao ni raia wa Marekani au wakazi halali wataruhusiwa kuomba kibali cha kazi kitakachodumu kwa miaka mitatu.
Wazazi tu walioishi Marekani kwa miaka mitano wataruhusiwa kuomba kibali hicho – takriban watu milioni nne wanakadiriwa kuwa na sifa hizo.
Ingawa mpango huo utaruhusu mamilioni ya watu kufanya kazi, haitotoa fursa ya kupata uraia au kupata haki zote sawa kama Mmarekani, alisema.
"Kama wewe ni mhalifu, utahamishwa. Kama una mpango wa kuingia Marekani kinyume na sheria, uwezekano wa kukamatwa na kurejeshwa ndio umeongezeka," alisema.
No comments:
Post a Comment