Monday 17 November 2014

DK WA SIERRA LEONE AFARIKI DUNIA KWA EBOLA



Martin Salia

Daktari kutoka Sierra Leone aliyekuwa akitibiwa kwa maradhi ya Ebola nchini Marekani amefariki dunia, hospitali ya Nebraska ilitangaza.

Martin Salia, ambaye ana uraia wa Marekani na amemwoa Mmarekani, aliwasili kupata matibabu kwenye jimbo hilo siku ya Jumamosi, akiwa katika hali mbaya sana.

Na siku ya Jumatatu asubuhi hospitali ilisema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 44 alifariki dunia.

Zaidi ya watu 5,000 wamefariki dunia katika mlipuko wa Ebola wa hivi karibuni – karibu wote Afrika magharibi. Dk Salia ni mtu wa pili kufa Marekani.

Raia wa Liberia Thomas Eric Duncan alifariki dunia huko Dallas mwezi uliopita baada ya kupata virusi hivyo mjini Monrovia.

Hali ya hatari ya taifa iliyotangazwa nchini Liberia iliisha wiki iliyopita na siku ya Jumapili, Rais Ellen Johnson Sirleaf alisema ana matumaini nchi hiyo haitokuwa na virusi hivyo  ifikapo Krismas.


No comments:

Post a Comment