Sunday, 16 November 2014

MATEKA WA MAREKANI 'AUAWA NA IS'



 Mr Kassig

Video iliyowekwa kwenye mtandao inadai kuonyesha wapiganaji wa kundi linalojiita Islamic Sate, IS likimwuua mfanyakazi wa shirika la kutoa msaada la Marekani aliyekuwa mateka, Abdul-Rahman Kassig.

Katika video hiyo, mpiganaji mmoja aliyejifunika sura amesimama pemebezoni mwa kichwa ambacho anasema ni cha Bw Kassig.

Marekani imesema inajaribu kuchunguza uhalali wa video hiyo, ambayo pia inaonyesha mauaji ya watu wengi wa majeshi ya Syria.

Bw Kassig, ambaye pia anajulikana kwa jina la Peter, alikamtwa mwaka jana.

Familia yake, inayoishi Marekani katika jimbo la Indiana, alisema walikuwa wanasubiri uthibitisho wa ripoti hizo za “mtoto wao mpendwa”  na hawakuwa na la ziada la kusema.

Kama kifo chake kitathibitishwa, kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa mateka wa tano wa kutoka nchi za  kimagharibi kuuawa na kundi la IS, ikifutaiwa na mauaji ya Waingereza Alan Henning na David Haines, na mwandishi wa habari wa Marekani James Foley na Steven Sotloff.


No comments:

Post a Comment